RASIMU YA KATIBA YA UMOJA WA WANAKISALE SECONDARY 2014

Imeandaliwa na
Kamati ya maandalizi ya rasimu ya Katiba ya UWAKISE
ü  DEODATH INYAS KIMARIO
ü  STEVEN DEOGRATIUS
ü  YUDATHADE RICHARD
ü  ELIZABETH PIUSI
ü  EMANOELA WILLIUM
ü  VICTORIA VENANCE
ü  ZENAS ALIFREDI
ü  MARCELINA ONESPHORI
ü  GASPER HUGHO KISARIKA

SURA YA KWANZA
UTANGULIZI

1.   (1)  JINA LA CHAMA.                                                                                                  
a)      “UMOJA WA WANAKISALE SECONDARY.”
b)      Kwa kifupi litatamkwa “ UWAKISE”

2.     MAKAO MAKUU YA CHAMA
Makao makuu ya chama yatakuwa DAR ES SALAAM – TANZANIA.

3.    ANUANI YA CHAMA ITAKUWA:-
UWAKISE
P O BOX ……., D’SALAAM
TANZANIA.
Email: ……………….

4.    MAHALI KITAKAPOFANYIA SHUGHULI ZAKE
UWAKISE - kitaendesha shughuli zake katika mkoa wa D’Salaam na baadae katika mikoa/Wilaya ambayo wanachama wataamua.

5.         MAUDHUI YA CHAMA (STATUS)
UWAKISE ni chama cha kujitolea kisicho cha kiserikali, kisiasa wala Kidini kinachojihusisha na shughuli za kijamii za kusaidiana katika maswala ya Ustawi wa jamii na maendeleo ya wanachama wake.

SURA YA PILI
MADHUMUNI YA CHAMA.

  1.  MADHUMUNI YA JUMLA (GENERAL OBJECTIVES).
 Kukuza uelewano baina ya wanachama  na kusaidiana kwa  hali na mali wakati wa   shida na raha, na kuwawezesha wanachama wake kuwa na uwezo wa kutatua matatizo  yao ya dharura na ya  kiuchumi kwa kupitia chama hiki.

7.  MADHUMUNI MAHUSUSI (SPECIFIC OBJECTIVES).
(1) USTAWI WA JAMII KWA WANACHAMA,
a)      Kudumisha uhusiano mwema kati ya wanachama kwa kutembeleana na kufahamiana kidugu.
b)      Kutoa rambirambi katika misiba inayomhusu mwanachama (Kama vile Kifo cha mwanachama, Mume, mke, mtoto wazazi wa mwanachama aliye sajiliwa.
c)      Kuwa na siku maalumu ya kufanya sherehe za chama kila mwaka kwa jinsi itakavyoamuliwa na wanachama.
d)      Kushirikiana kwa hali na mali katika masuala ya Ugonjwa na harusi.
e)      Kuanzisha chama cha kuweka na kukopa ili kuwasaidia wanachama wake kupata mikopo ki urahisi na yenye riba nafuu, hii itasaidia kuinua hali ya kiuchumi kwa wanachama wa chama hiki.
f)        Kuwa na miradi midogomidogo itakayosaidia kukuza mfuko wa chama.
                       
(2) KUDUMISHA UTAMADUNI
a)      Kutoa fursa sawa kwa wanachama wote na kuondoa kabisa ubaguzi wa kijinsia bila kujali hali ya mwanachama mmoja mmoja, wanachama wote watashirikishwa sawa katika shughuri zote za chama.
b)      Kuwasaidia na kuwajali wasiojiweza kwa kuwatembelea mahali walipo na kuwafariji kwa hali na mali.
c)      Kudumisha mila na desturi za kitanzania kwa kujali na kulinda tamaduni zetu. (To Develop Cultural and traditional Values)


SURA YA TATU.
UANACHAMA
  8. (1) KUJIUNGA NA CHAMA. (ELIGILITY CRETERIA) NA AINA ZA UANACHAMA
a)      Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18 ama zaidi anaweza kujiunga na chama ili mradi awe na akili timamu na akubaliane na Masharti na kanuni za chama.
b)      Mke na Mume wata hesabiwa kama mwanachama mmoja.
c)      Mwanamume/mwanamke ambaye hajaolewa atahesabiwa kama mwanachama mmoja.
d)      Mume mwenye wake zaidi ya mmoja ni mke mmoja tu ndiye atakayehesabika uanachama. Mke/wake wengine wataingia kama wanachama wengine.
e)      Kutakuwa na wanachama wa heshima, ambao uanachama huu hupewa mtu mwenye hadhi na anayeleta amslahi ya kim-saada kwenye chama bila kujali kama ni wa ndani au wa nje.

 (2 ) UTARATIBU WA KUJIUNGA NA CHAMA.
a)      Mtu yeyote atajiunga na chama kwa kujaza fomu maalumu ya maombi  na kupitisha kwa Katibu Mkuu, na kujadiliwa na halmashauri kuu na kisha kudhibitishwa na mkutano mkuu.
b)      Uanachama wa mtu utaanza kutambuliwa mara tu baada ya  kulipa kiingilio na ada alizo amriwa na chama.
c)      Mwanachama aliyefukuzwa anaweza kuomba kurudia uanachama baada kujaza fomu maalumu ya maombi kupitisha kwa Katibu Mkuu na Kupitiwa Halmashauri Kuu na anaweza kukubaliwa / kukataliwa na mkutano mkuu endapo utaridhika kuwa amejirekebisha / kutojirekebisha.
d)      Mwanachama aliyejiachisha uanachama kwa sababu ya matatizo kama vile kuachishwa kazi, kuugua muda mrefu, uhamisho wa kikazi nje ya (Mkoa / Wilaya) maeneo kinapofanyiakazi chama na hivyo kushindwa kutekeleza masharti yaliyomo katika kifungu 9(1) (a) mpaka 9(1) (g) ya katiba hii, akiomba uanachama ataruhusiwa kwa kulipa kiingilio kinacholingana na michango ya mwaka mmoja baada ya kutoa uthibitisho.
e)      Mwanachama ataweza kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe na kupeleka taarifa ya maandishi kwa Katibu Mkuu.
f)       Mwanachama ataachishwa uanachama endapo vitendo na kauli zake ni za kukiuka katiba kama vile kuchochea migogoro au ya kuleta mitafaruku katika chama.
g)      Mwanachama atakuwa amejisimamisha mwenyewe uanachama ikiwa atashindwa kulipa ada kwa miezi mitatu au/na kutohudhuria vikao vinne vya chama mfululizo
h)      Kwa vyovyote vile mwanachama aliyeacha/achishwa uanachama hatarudishiwa fedha yeyote.
i)        Mwanachama asipolipa ada kwa muda wa miezi mitatu (3) hatakuwa na haki kuhudumiwa na chama katika matatizo yake.
j)        Mwanachama asipolipa ada kwa muda wa Miezi mitatu (3) atakuwa amejiondoa uanachama mwenyewe.
k)      Endapo mtu anayetaka kujiunga na chama na hayupo Dar es salaam lazima awe na mdhamini ambaye ni mwanachama hai.
l)        Endapo mtu anayetaka kujiunga na chama sio mhitimu wa Kisale Sekondari lazima awe na mdhamini ambaye ni mwanachama hai.


SURA YA  NNE.
WAJIBU.( RESPONSIBILITIES)

9. (1) WAJIBU WA MWANACHAMA KWA CHAMA
a)       Kulipa kiingilio cha uanachama kwa kiwango kilichowekwa na chama. 
b)      Kulipa ada ya uanachama kwa kiwango kilichowekwa na chama.
c)      Kuchangia mfuko wa chama kama itatokea majanga yakawa mengi na kusababisha mfuko kupungua kiasi cha kutoweza kutoa huduma.
d)      Kuhudhuria vikao vinavyomhusu bila kukosa.
e)       Kushiriki misiba na shughuli zote zinazowahusu wanachama bila kukosa.
f)        Kuheshimu Katiba na maelekezo ya viongozi.
g)      Kuhudhuria sherehe zitakazo pangwa na chama kwa ajili ya kukuza uelewano wa wanachama.

 (2) WAJIBU WA CHAMA KWA WANACHAMA
a)      Kutoa rambirambi kama ilivyoainishwa katika kifungu 7(1) (b) cha madhumuni ya chama (Kumpunguzia mwanachama makali ya gharama za msiba.)
b)      Kwa kupitia viongozi, kitahamasisha wanachama kumsaidia kwa hali na mali mwanachama kama ilivyoainishwa katika kifungu 7(1) (d) cha katiba hii.          
c)      Kuchangia sherehe za mwaka za chama kutoka mfuko wa chama Kwa kiasi kilichoamriwa na chama.


SURA YA  TANO.
UONGOZI WA CHAMA
10. (1) MUUNDO WA UONGOZI WA CHAMA
      Chama kitakuwa na viongozi wafuatao:
a)                  Mwenyekiti,
b)                   Makamu Mwenyekiti,
c)                   Katibu Mkuu,
d)                   Katibu Msaidizi,
e)                  Mweka Hazina,

    (2)   SIFA ZA KIONGOZI
a)      Mwanachama yeyote mwenye umri usiopungua miaka Kumi na 18 na awe akili timamu anaweza kugombea uongozi.
b)      Awe ni Mtunza siri za chama/kikundi.
c)      Awe radhi kufanya kazi kwa kujitolea.

11.  NAMNA YA KUPATA VIONGOZI
    Viongozi watapatikana kwa kuchaguliwa na wanachama katika mkutano mkuu wa wanachama wote kwa kura za siri.

Viongozi hawa watasaidiwa na Kamati mbili za Utendaji. Kwa ujumla wao watafanya Halmashauri Kuu ya wajumbe kumi na moja.

12.  UCHAGUZI
      Viongozi wa chama watachaguliwa kila baada ya mwaka mmoja, na Viongozi waliomaliza muda wao wanaweza kugombea tena.
Mwenyekiti kupitia Halmashauri kuu atakuwa na uwezo kumteua mwanachama yeyote kuingia katika kamati za uongozi ndani ya chama, kama vile Mkaguzi wa mahesabu ya chama,
a)                  Mkutano mkuu utapendekeza Wanachama wawili kugombea nafasi za juu za Uongozi na kupigiwa kura na wajumbe wote wa mkutano mkuu. Matokeo yatatangazwa kabla ya uchaguzi wa ngazi inayofuata atakayepata kura nyingi zaidi atatangazwa mshindi.
b)                  Majina kumi na mbili ya wanachama yatapendekezwa na kupigwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu ili kupata wajumbe tano wa Halmashauri Kuu.
c)                  Ikiwa kiongozi aliyechaguliwa atajiuzulu au kuondolewa madarakani kwa sababu zozote zile Mkutano mkuu wa dharura utaitishwa katika kipindi cha miezi mitatu (3) ili kufanya uchaguzi na kujaza nafasi iliyowazi.
d)                  Ikiwa kiongozi hatakuwepo katika mkoa ambao chama kinaendeshea shughuli zake kwa kwa vikao vitatu mfululizo kwa sababu za kikazi/masomo/ugonjwa au utalii mkutano mkuu wa dharura utaitishwa ili kufanya uchaguzi mara baada ya kipindi hicho.
e)                  Kura zitapigwa wa siri chini ya usimamizi wa Mwenyekiti au                                    Mwenyekiti wa muda atakaechaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi.


SURA YA SITA
MAJUKUMU YA VIONGOZI WA CHAMA
13.  VIONGOZI WAKUU NA MAJUKUMU YAO.
(1) KUTAKUA NA MWENYEKITI WA CHAMA:           
a)      Kuhakikisha kuwa Katiba inafuatwa.             
b)      Kuongoza Mikutano.
c)      Kusimamia shughuli zote za utendaji wa Chama.
d)      Atawajibika kwa Mkutano mkuu  ya Chama
e)      Atakuwa mtia saini katika akaunti ya fedha za chama.
f)        Atakuwa mtia saini katika mikataba yote inayohusu chama.
g)      Atakuwa ndie msimamizi mkuu wa shughuli zote za chama

          (2) KUTAKUWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA.
a)      Ndiye atakae kuwa mtendaji mkuu wa shughuli za chama na atawajibika kwa Mwenyekiti wa Chama.
b)      Kuitisha na kuandaa mikutano kwa mujibu wa katiba.Kutunza kumbukumbu na nyaraka zote za chama.
c)      Atapokea maombi ya Wanachama wapya na kuwasilisha kwenye Halmashauri kuu kwa kujadiliwa.
d)      Atapokea hoja mbalimbali za wanachama na kuzifanyia kazi.
e)      Kuwajulisha kimaandishi wanachama waliofukuzwa na Mkutano Mkuu ama wale waliopoteza uanachama kwa kutozingatia maagizo ya katiba kama ilivyoainishwa katika vifungu 9(1) (a) hadi 9(1) (g).
f)        Atakuwa mtia saini katika akaunti ya fedha za chama.


(3)KUTAKUWA NA MTUNZA HAZINA WA CHAMA.
a)      Kukusanya michango na kutunza kumbukumbu za fedha.
b)      Kufanya malipo yaliyoidhinishwa kwa mujibu wa katiba.
c)      Atawajibika kutayarisha bajeti ya mwaka ya chama.
d)      Kutoa taarifa za mapato na Matimizi ya fedha za chama katika mikutano yote.
e)      Atawajibika kutoa “bank statement” inayoonyesha mapato na matumizi tokea mkutano mkuu wa mwisho ulipofanyika.
f)        Atakuwa mtia saini katika akaunti ya fedha za chama.
g)      Atawajibika kwa Mwenyekiti wa chama kwa mujibu wa katiba.

14.    VIONGOZI WAKUU WAANDAMIZI NA MAJUKUMU YAO.
  (1) KUTAKUWA NA MAKAMU MWENYEKITI
a)      Kumsaidia Mwenyekiti na kufanya kazi zote kama Mwenyekiti Hayupo.
b)      Endapo Mwenyekiti atajiuzulu au kuondolewa madarakani kwa sababu zozote zile, Makamu Mwenyekiti atakaimu nafasi hiyo kwa mujibu wa kijifungu 12(d) cha Katiba hii.
c)      Endapo Mwenyekiti hata kuwepo katika vikao vitatu kwa sababu za kikazi/masomo/ugonjwa au utalii, Makamu mwenyekiti atakaimu nafasi hiyo na mara baada ya kipindi hicho uchaguzi utafanywa kwa mujibu wa kifungu 12(e) cha katiba hii.

  (2) KUTAKUWA NA MAKAMU KATIBU MKUU.
a)      Kumsaidia Katibu Mkuu katika majukumu yake yote.
b)      Endapo Katibu Mkuu atajiuzulu au kuondolewa madarakani kwa sababu zozote zile, Makamu katibu mkuu atakaimu nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu 12(d) cha Katiba hii.
c)      Endapo Katibu Mkuu hatakuwepo katika vikao vitatu mfululizo kwa sababu za kikazi/masomo/ugonjwa au utaliii, Katibu Msaidizi atakaimu nafasi hiyo na mara baada ya kipindi hicho uchaguzi utafanywa kwa mjibu wa kijifungu 12(e) cha Katiba hii.
d)      Atawajibika kwa katibu mkuu kwa mujibu wa katiba=

15. KIPINDI CHA KUWEPO MADARAKANI.
      Baada ya kuchaguliwa, viongozi watakaa madarakani kwa vipindi (Viwili/mitatu/mine/mitano) iwapo kiongozi atashinda katika uchaguzi wa awamu nyingine.
16.  HALIMASHAURI KUU YA CHAMA
(1)   WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU;
a)                  Mwenyekiti
b)                  Katibu mkuu
c)                  Mweka Hazina.
d)                  Makamu Mwenyekiti.
e)                  Katibu Msaidizi.
f)                    Wajumbe tano (5) watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Chama.

(2)   KAZI ZA HALMASHAURI KUU
a)                  Watasimamia na kutekeleza majukumu yote kama yatakayoamuliwa na Mkutano Mkuu.
b)                  Kubuni sera za chama na kutoa dira ya chama ili kudumisha uhai Wake.
c)                  Kuwajadili wanachama wapya na kupeleka mapendekezo mbele ya Mkutano Mkuu.
d)                  Kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote na kumchukulia hatua za Kisheria itakapobidi kwa makubaliano ya wajumbe wasiopungua theluthi mbili.
e)                  Kuwasilisha mapendekezo ya kufukuzwa kiongozi au viongozi waliosimamishwa mbele ya Mkutano Mkuu.
f)                    Kuwasimamisha uanachama watu watakaokiuka katiba na kupeleka mapendekezo ya kuwafukuza uanachama mbele ya Mkutano Mkuu.

17.  KAMATI ZA UTENDAJI NA KAZI ZAKE
(1)   Kutakuwa na Kamati mbili za Utendaji za Halmashauri Kuu ya Chama ambazo ni
a)       Kamati ya fedha na uchumi, kamati hii itakuwa na wajumbe sita na itawajibika kwa Mwenyekiti wa Chama. Wajumbe watakuwa Katibu Mkuu, Mweka hazina na wajumbe watatu wa halmashauri kuu.
b)      Kamati ya ustawi wa jamii na sherehe.kamati hii itaongozwa na wajumbe halmashauri kuu,
(2)   kazi kuu ya kamati  ya ustawi wa jamii na sherehe hii ni:-
a)      Kuhamasisha wanachama kutoa michango inayowahusu
b)      Kuhamasisha wanachama kuwasaidia wanachama walio wagonjwa mahututi.
c)      Kuhamasisha wanachama kushiriki katika Harusi na sherehe za mwanachama.
d)      Kuratibu sherehe za kuadhimisha mwaka kama ilivyoainishwa katika kifungu  7(1) (c) Cha katiba hii.

18. MIKUTANO YA CHAMA NA KAZI ZAKE.
a)      Kutakuwa na Mkutano Mkuu utakaofanyika mara moja kwa mwaka
b)      Kutakuwa na mkutano wa Halmashauri Kuu kila baada ya miezi miwili.
c)      Kutakuwa na mkutano wa wanachama wote kila baada ya miezi mitatu.
d)      Kutakuwa na mkutano wa uchaguzi mkuu mara moja kila baada ya mwaka mmoja.
e)      Mkutano wa dharura unaweza kuitishwa endapo viongozi ama asilimia hamsini (50%) ya wanachama wataona ipo haja ya kufanya hivyo.

19. KAZI ZA MKUTANO MKUU.
a)      Kupokea taarifa mbalimbali za kiutendaji.
b)      Kutoa maamuzi yahusuyo uhai na ubora wa chama.
c)      Kubadili kifungu cha Katiba endapo itaonekana ni lazima kufanya hivyo.
d)      Kuthibitisha kuachishwa au kufukuzwa Uanachama mtu yeyote.
e)      Kufanya uchaguzi  viongozi wa chama.
f)        Kuthibitisha kuachishwa au kufukuzwa kwa kiongozi.
g)      Kuthibitisha uanachama wa mwombaji mpya.
h)      Kuchagua Viongozi wa ngazi za juu pamoja na Halmashauri Kuu.
           


SURA YA SABA
FEDHA ZA CHAMA.
20. UHIFADHI WA FEDHA ZA CHAMA
 (1) Fedha yote ya chama itatunzwa katika Bank ambayo itateuliwa na wanachama wa chama hiki na kusimamiwa na Mtunza Hazina.
(2)  Chama kitakuwa na watia saini katika Bank ambao ni Mwenyekiti, Katibu Mkuu na mweka hazina.

21.  VYANZO VYA MAPATO
(1) Upatikanaji wa fedha
a)         Kiingilio cha uanachama.
b)         Ada za kila mwezi za uanachama.
c)         Michango ya dharura.
d)         Mauzo ya mali za chama kama vile katiba.
e)         Faini mbalimbali.
            (2) Chama kitaanzisha na kubuni miradi ya kiuchumi na kutoa huduma kwa wanachama kwa kuwa na chama cha kuweka na kukopa kitakachotoa mikopo kwa riba nafuu kwa wanachama wake.

22.  UKUSANYAJI WA FEDHA ZA CHAMA
Mwanachama ataweka fedha za kiingilio na michango mingine katika Bank na kuwasilisha hati ya malipo ya Bank kwa Mweka Hazina na kupewa Stakabadhi.

23. MATUMIZI YA MFUKO WA CHAMA
(1) Kutoa rambirambi kwa wafiwa kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 9 (2) (a)
(2) Kugharimia shughuli za Mkutano Mkuu kwa kiwango kilichoamuliwa na Mkutano Mkuu     
(3)Kugharamia shughuli za Halmashauri kuu kwa kiwango kilichoamuliwa na Mkutano Mkuu
(4)Kugharimia uchukuaji na upelekaji wa fedha kwa mfiwa kwa kiwango kilichoamuliwa na Mkutano Mkuu
(5)Kugharamia shughuli za msingi za uendeshaji wa chama kama vile upashanaji habari kupitia magazeti na redio, ununuzi wa karatasi, kalamu, stemp, bahasha na kutoa nakala za taarifa za chama. Usimamizi utakuwa chini ya Halmashauri Kuu.
(6) Kugharamia shughuli za sherehe za chama kwa 25% ya bajeti ya sherehe na  itavyopitishwa na Mkutano Mkuu.

24. UPASHANAJI TAARIFA
Mwanachama mwenye taarifa ya msiba, Harusi, au ugonjwa atawajibika kutoa taarifa kwa mjumbe wa halmashauri kuu, viongozi au wanachama walio karibu naye kwa njia yoyote kwa lengo la kuwashirikisha wanachama.



SURA YA NANE.
MAMBO YA JUMLA YA KATIBA.
25. KUBADILI KATIBA,
 Kwa kuwa katiba sio maandiko matakatifu, wanachama kupitia taratibu zake wanaruhusiwa kuifanyia marekebisho ya kuiongezea au kupunguza baadhi ya vipengele vilivyopitwa na wakati

26.  USULUHISHI:
 Migogoro ya ndani ya chama itapatiwa usuluhishi na  halmashauri kuu  ya chama, endapo litashindikana kutatuliwa na halmashauri kuu basi busara ya waasisi itatumika kutatua mgogoro huo.

26.  KUFUTWA KWA CHAMA(RESOLUTION);
Chama hiki kitafutwa kwa maamuzi ya sheria za nchi na chama chenyewe ikiwa:Kama kitatenda makosa yanayokiuka sheria za nchi, kama vile kwenda kinyume na sera za vyama na sera ya taifa ya mashirika yasiyo ya kiserikali

27.  MALI ZA CHAMA ENDAPO CHAMA KITAFUTWA.
(1)               Kuteua Mfilisi atakayesimamia namna mali hizo zitakavyotumika au kuzigawa,
(2)               Kulipia madeni ya chama kabla ya kuanza kugawa au kuhamishiwa kwa asasi nyingine za walengwa

TAMKO RASMI LA MKUTANO MKUU WA KWANZA ULIOFANYIKA TAREHE 31/08/2014 NA MAREKEBISHO YA KWANZA YA KATIBA YALIYOFANYIKA TAREHE__________________.
Katiba hii ni halali na mali ya chama
Katiba hii itatumika Kwa ushahidi wa kisheria.
Badiliko lolote litakalofanywa na mkutano mkuu litaheshimiwa na viongozi
na wanachama.
Viongozi Na wanachama watailinda na kuienzi kama dira ya shughuli za
Chama.

MWISHO

KANUNI ZA UENDESHAJI WA CHAMA

UTANGULIZI

Mkutano mkuu wa UWAKISE uliofanyika tarehe …… na ule wa tarehe_________ uliamua kwa kauli moja kuwa baadhi ya vipengele katika katiba viwekewe na kuboresha Kanuni zilizopo.
Kanuni hizi zinaweza kufanyiwa marekebisho na mkutano mkuu wa UWAKISE pale inapobidi na zitaendelea kutumika mpaka tarehe ambayo mkutano mkuu wa UWAKISE utakapoamua vinginevyo.
Madhumuni ya Kanuni hizi ni kutoa mwongozo kwa viongozi na wanachama katika kutekekeza wajibu wao kwa chama kwa jumla.Kanuni zinalenga katika maeneo ambayo yanaweza yakapitwa na wakati katika kiipindi kifupi kama vile ada ya kujiunga na uanachama, ada ya kila mwezi na kiasi cha fedha zitakazotolewa kwa mwanachama kama rambirambi atakapopata msiba. Aidha, Kanuni zinafafanua adhabu/faini atakayopewa mwanachama anapoenda kinyume na katiba. Kuwepo kwa kanuni kutasaidia kuwa na katiba imara ambayo haifanyiwi marekebisho ya mara kwa mara na hivyo kujenga mazoea ya kufanya hivyo.
Kanuni hizi msingi wake mkuu ni katiba ya UWAKISE na si vinginevyo.
WAJIBU WA MWANACHAMA KWA CHAMA
Katika kuhakikisha kuwa chama kinakuwa hai na kinatekeleza majukumu yake kikamilifu, na kwa kuzingatia kifungu kikubwa Na. 9 cha katiba ya UWAKISE, na kufafanuliwa na vifungu vidogo Na. 9(1) (a)  na 9(1) (b) vya katiba hiyo pamoja na mambo mengine, mwanachama atatakiwa kutekeleza mambo yafuatayo:
i)                    Kulipa kiingilio ambacho ni Tsh. 50,000/=
ii)                   Kulipa ada ya uanachama ya kiasi cha Tsh. 5,000/= kila mwezi
Mwanachama atakuwa na uhuru wa kulipa kwa miezi yoyote anayotaka au mwaka mzima au zaidi.
iii)                 Kwa mujibu wa kifungu No. 9(1) (d) hadi 9(1) (g) vya katiba hiyo mwanachama
anawajibika kuhudhuria vikao vinavyo mhusu bila kukosa
asipohudhuria kikao bila kutoa taarifa maalum kwa katibu au katibu msaidizi atawajibika kulipa faini ya shilingi 3,000/= (Elfu tatu tuu).
iv)                 Atakayechelewa kufika kwenye kikao nusu saa baada ya muda uliopangwa atatozwa Tsh. 2000/= (Elfu moja).
v)                  Asipolipa faini zilizotajwa katika vifungu (iii) na (iv) hapo juu, fedha hizo zitakatwa kwenye malipo yake ya ada ya kila mwezi.
vi)                Ataachishwa uanachama ikiwa hatahudhuria mikutano minne mfululizo inayohusu bila sababu za msingi.

WAJIBU WA CHAMA KWA WANACHAMA
Kufuatana na kifungu No. 4.0 cha Katiba ya UWAKISE na kufafanuliwa na kijifungu kidogo Na..4.2.1 cha Katiba hii, ili kupunguza makali ya msiba, chama kitatoa rambiramni katika misiba ifuatayo:
i)                    Endapo mwanachama  ataoa au kuolewa cha kitatoa Tsh. 500,000/=
ii)                   Endapo mwanachama atafariki chama kitatoa Tsh. 800,000/=
iii)                 Kufiwa na Mume/Mke/Mtoto, chama kitatoa rambirambi ya Tsh. 500,000/= (Laki tano tu).
iv)                 Kufiwa Baba/Mama, chama kitatoa rambirambi ya Tsh. 400,000/= 
(Laki nne tu)
v)                  Kwa misiba ya Baba au Mama mzazi inayohusu wanachama zaidi ya mmoja chama kitatoa huduma  kwa kila mwanachama, kwani uanachama si wa familia ya baba au mama mmoja ila ni wa mwanachama na familia yake( mume na mke.)
MATUMIZI YA MFUKO WA CHAMA
Kifungu Na. 9.4.2 hadi 9.4.6 cha Katiba ya UWAKISE, mbali na misiba, kinaainisha maeneo mengine ambayo fedha za chama zitatumika. Maeneo hayo na gharama zake ni kama yafuatayo:-
i)                    Katika sherehe za chama za mwaka, mfuko wa chama utachangia kiasi kilichopungua.
ii)                  Kugharamia shughuli za mkutano mkuu, kwa kiwango kisichozidi Tsh. 120,000/=
iii)                Vikao vya chama/miktao ya dharura kwa kiwango kisichozidi 50,000/=
iv)                 Kugharamia shughuli za Halmashauri kuu, kwa kiwango kisichozidi Tsh. 50,000/=.
v)                  Kugharamia shughuli za Kamati ndogo za Halmashauri kuu, kwa kiwango kisichozidi Tsh. 25,000/=.
vi)                 Kugharamia uchukuaji na upelekaji pesa kwa Mfiwa kwa kiwango
                    Kisichozidi Tsh. 30,000/=
vi)        Kugharamia ununuzi wa karatasi, kalamu, stamp, bahasha, kutoa nakala za taarifa za chama na mawasiliano ya simu kama itatokea.


MWISHO

UWAKISE
 
P.O. BOX ……….,
DAR ES SALAAM

FOMU YA MAOMBI YA UANACHAMA

Mimi………………………………………wa    Mtaa………………………………
P. O. Box………………………….
Ninaomba kujiunga na Chama cha UWAKISE, umri wangu ni 
miaka ……..nimeoa / nimeolewa / sijaoa /sijaolewa. Nipo tayari kufuata taratibu za chama kwa mujibu ya katiba ya chama hiki, na nipo tayari kutoa kiingilio na michango ya kila mwezi kama ilivyoanishwa katika katiba na kanuni za chama.
Nina watoto wafuatao.
            JINA                                       UMRI               JINA                                       UMRI
1……………………………              …….               2………………………….     ……..
3……………………………              …….               4………………………….     ……..
5……………………………              …….               6…………………………      ……..
Mimi na Mke/Mme wangu kwa hapa DSM tunaishi…………………………..
Wazazi wetu wapo hai / hawapo hai.
Baba na mama Mzazi anaishi…………………………………….pia baba na mama mkwe wanaishi…………………………………………………………….
UTHIBITISHO WA MUOMBAJI.
Ninathibitisha kwamba yote niliyoeleza katika fomu hii ni ya kweli tupu.
Ninahidi kutoa kiingilio cha Tshs…………………..na ada  ya kila mwezi kwa kipindi cha miezi………………ambayo ni Tshs………………..
Sahihi na tarehe  ya Muombaj………………………………………………….
Imepitishwa / Haikupitishwa kwa sababu…………………………………………
……………………………………………………………………………………………..
NB: Endapo kama nitafariki au kupatwa na tatizo mtu wangu wa karibu au mwakilishi wangu ni ………………………………. Ambaye ni …………………………………. Kwangu.

    _____________________                                              _____________________
    Sahihi ya Katibu Mkuu.                                     Sahihi ya Mwenyekiti

*Maombi yenye taarifa ya uongo haitapitishwa,
(Gharama ya fomu hii ni Tshs 1000/= tuu- zijazwe nakala
mbili) (Ambatanisha