Kamati ya maandalizi ya rasimu ya Katiba
ya UWAKISE
ü DEODATH
INYAS KIMARIO
ü STEVEN
DEOGRATIUS
ü YUDATHADE
RICHARD
ü ELIZABETH
PIUSI
ü EMANOELA
WILLIUM
ü VICTORIA
VENANCE
ü ZENAS
ALIFREDI
ü MARCELINA
ONESPHORI
ü GASPER
HUGHO KISARIKA
SURA
YA KWANZA
UTANGULIZI
1.
(1) JINA LA CHAMA.
a)
“UMOJA
WA WANAKISALE SECONDARY.”
b) Kwa kifupi
litatamkwa “
UWAKISE”
2. MAKAO MAKUU YA CHAMA
Makao makuu
ya chama yatakuwa DAR ES SALAAM – TANZANIA.
3. ANUANI YA CHAMA ITAKUWA:-
UWAKISE
P O BOX ……., D’SALAAM
TANZANIA.
Email: ……………….
4. MAHALI KITAKAPOFANYIA SHUGHULI ZAKE
UWAKISE - kitaendesha shughuli zake katika mkoa wa
D’Salaam na baadae katika mikoa/Wilaya ambayo wanachama wataamua.
5. MAUDHUI YA CHAMA (STATUS)
UWAKISE ni chama cha kujitolea kisicho cha kiserikali,
kisiasa wala Kidini kinachojihusisha na shughuli za kijamii za kusaidiana
katika maswala ya Ustawi wa jamii na maendeleo ya wanachama wake.
SURA
YA PILI
MADHUMUNI YA
CHAMA.
- MADHUMUNI YA JUMLA (GENERAL OBJECTIVES).
Kukuza uelewano
baina ya wanachama na kusaidiana
kwa hali na mali wakati wa shida na raha, na kuwawezesha wanachama wake
kuwa na uwezo wa kutatua matatizo yao ya
dharura na ya kiuchumi kwa kupitia chama
hiki.
7. MADHUMUNI MAHUSUSI (SPECIFIC OBJECTIVES).
(1) USTAWI
WA JAMII KWA WANACHAMA,
a)
Kudumisha uhusiano mwema kati ya
wanachama kwa kutembeleana na kufahamiana kidugu.
b)
Kutoa rambirambi katika misiba inayomhusu mwanachama (Kama vile Kifo cha
mwanachama, Mume, mke, mtoto wazazi wa mwanachama aliye sajiliwa.
c)
Kuwa na siku maalumu ya kufanya
sherehe za chama kila mwaka kwa jinsi itakavyoamuliwa na wanachama.
d)
Kushirikiana kwa hali na mali katika
masuala ya Ugonjwa na harusi.
e)
Kuanzisha chama cha kuweka na kukopa
ili kuwasaidia wanachama wake kupata mikopo ki urahisi na yenye riba nafuu, hii
itasaidia kuinua hali ya kiuchumi kwa wanachama wa chama hiki.
f)
Kuwa na miradi midogomidogo
itakayosaidia kukuza mfuko wa chama.
(2) KUDUMISHA UTAMADUNI
a)
Kutoa fursa sawa kwa wanachama wote
na kuondoa kabisa ubaguzi wa kijinsia bila kujali hali ya mwanachama mmoja
mmoja, wanachama wote watashirikishwa sawa katika shughuri zote za chama.
b)
Kuwasaidia na kuwajali wasiojiweza
kwa kuwatembelea mahali walipo na kuwafariji kwa hali na mali.
c)
Kudumisha mila na desturi za
kitanzania kwa kujali na kulinda tamaduni zetu. (To Develop Cultural and
traditional Values)
SURA
YA TATU.
UANACHAMA
8. (1) KUJIUNGA NA CHAMA. (ELIGILITY
CRETERIA) NA AINA ZA UANACHAMA
a) Mtu yeyote
mwenye umri wa miaka 18 ama zaidi anaweza kujiunga na chama ili mradi awe na
akili timamu na akubaliane na Masharti na kanuni
za chama.
b)
Mke na Mume wata hesabiwa kama
mwanachama mmoja.
c)
Mwanamume/mwanamke ambaye hajaolewa
atahesabiwa kama mwanachama mmoja.
d)
Mume mwenye wake zaidi ya mmoja ni
mke mmoja tu ndiye atakayehesabika uanachama. Mke/wake wengine wataingia kama
wanachama wengine.
e)
Kutakuwa na wanachama wa heshima,
ambao uanachama huu hupewa mtu mwenye hadhi na anayeleta amslahi ya kim-saada
kwenye chama bila kujali kama ni wa ndani au wa nje.
(2 ) UTARATIBU WA KUJIUNGA NA CHAMA.
a)
Mtu yeyote atajiunga na chama kwa kujaza fomu maalumu ya maombi na kupitisha kwa Katibu Mkuu, na kujadiliwa
na halmashauri kuu na kisha kudhibitishwa
na mkutano mkuu.
b)
Uanachama wa mtu utaanza kutambuliwa
mara tu baada ya kulipa kiingilio na ada
alizo amriwa na chama.
c)
Mwanachama aliyefukuzwa anaweza
kuomba kurudia uanachama baada kujaza fomu maalumu ya maombi kupitisha kwa Katibu Mkuu na Kupitiwa Halmashauri Kuu
na anaweza kukubaliwa / kukataliwa na
mkutano mkuu endapo utaridhika kuwa amejirekebisha / kutojirekebisha.
d)
Mwanachama aliyejiachisha uanachama
kwa sababu ya matatizo kama vile kuachishwa kazi, kuugua muda mrefu, uhamisho
wa kikazi nje ya (Mkoa / Wilaya) maeneo kinapofanyiakazi chama na hivyo
kushindwa kutekeleza masharti yaliyomo katika kifungu 9(1) (a) mpaka 9(1) (g)
ya katiba hii, akiomba uanachama ataruhusiwa kwa kulipa kiingilio
kinacholingana na michango ya mwaka mmoja baada ya kutoa uthibitisho.
e) Mwanachama
ataweza kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe na kupeleka taarifa ya maandishi kwa Katibu Mkuu.
f) Mwanachama
ataachishwa uanachama endapo vitendo na kauli zake ni za kukiuka katiba kama
vile kuchochea migogoro au ya kuleta mitafaruku katika chama.
g)
Mwanachama atakuwa amejisimamisha mwenyewe
uanachama ikiwa atashindwa kulipa ada kwa miezi mitatu au/na kutohudhuria vikao
vinne vya chama mfululizo
h)
Kwa vyovyote vile mwanachama
aliyeacha/achishwa uanachama hatarudishiwa fedha
yeyote.
i)
Mwanachama asipolipa ada kwa muda wa miezi mitatu (3)
hatakuwa na haki kuhudumiwa na chama katika matatizo yake.
j)
Mwanachama asipolipa ada kwa muda wa Miezi mitatu (3) atakuwa amejiondoa uanachama
mwenyewe.
k)
Endapo mtu anayetaka kujiunga na
chama na hayupo Dar es salaam lazima awe na mdhamini ambaye ni mwanachama hai.
l)
Endapo mtu anayetaka kujiunga na
chama sio mhitimu wa Kisale Sekondari lazima awe na mdhamini ambaye ni
mwanachama hai.
SURA
YA NNE.
WAJIBU.(
RESPONSIBILITIES)
9. (1)
WAJIBU WA MWANACHAMA KWA CHAMA
a)
Kulipa kiingilio cha uanachama kwa kiwango
kilichowekwa na chama.
b)
Kulipa ada ya uanachama kwa kiwango
kilichowekwa na chama.
c)
Kuchangia mfuko wa chama kama
itatokea majanga yakawa mengi na kusababisha mfuko kupungua kiasi cha kutoweza
kutoa huduma.
d) Kuhudhuria
vikao vinavyomhusu bila kukosa.
e) Kushiriki misiba na shughuli zote zinazowahusu
wanachama bila kukosa.
f)
Kuheshimu Katiba na maelekezo ya viongozi.
g)
Kuhudhuria sherehe zitakazo pangwa
na chama kwa ajili ya kukuza uelewano wa wanachama.
(2) WAJIBU WA CHAMA KWA WANACHAMA
a) Kutoa
rambirambi kama ilivyoainishwa katika kifungu 7(1) (b) cha madhumuni ya chama (Kumpunguzia mwanachama makali ya gharama za msiba.)
b) Kwa kupitia
viongozi, kitahamasisha wanachama kumsaidia kwa hali na mali mwanachama kama
ilivyoainishwa katika kifungu 7(1) (d)
cha katiba hii.
c) Kuchangia
sherehe za mwaka za chama kutoka mfuko wa chama Kwa kiasi kilichoamriwa na
chama.
SURA
YA TANO.
UONGOZI WA
CHAMA
10. (1)
MUUNDO WA UONGOZI WA CHAMA
Chama
kitakuwa na viongozi wafuatao:
a)
Mwenyekiti,
b)
Makamu
Mwenyekiti,
c)
Katibu
Mkuu,
d)
Katibu
Msaidizi,
e)
Mweka Hazina,
(2)
SIFA ZA KIONGOZI
a)
Mwanachama yeyote mwenye umri
usiopungua miaka Kumi na 18 na awe akili timamu anaweza kugombea uongozi.
b)
Awe ni Mtunza siri za chama/kikundi.
c)
Awe radhi kufanya kazi kwa
kujitolea.
11. NAMNA YA KUPATA VIONGOZI
Viongozi
watapatikana kwa kuchaguliwa na wanachama katika mkutano mkuu wa wanachama wote
kwa kura za siri.
Viongozi hawa watasaidiwa na Kamati mbili za Utendaji.
Kwa ujumla wao watafanya Halmashauri Kuu ya wajumbe kumi na moja.
12. UCHAGUZI
Viongozi
wa chama watachaguliwa kila baada ya mwaka
mmoja, na Viongozi waliomaliza muda wao wanaweza kugombea tena.
Mwenyekiti kupitia Halmashauri kuu atakuwa na uwezo
kumteua mwanachama yeyote kuingia katika kamati za uongozi ndani ya chama, kama
vile Mkaguzi wa mahesabu ya chama,
a)
Mkutano mkuu utapendekeza Wanachama wawili kugombea nafasi za juu za Uongozi na kupigiwa kura na
wajumbe wote wa mkutano mkuu. Matokeo yatatangazwa kabla ya uchaguzi wa ngazi
inayofuata atakayepata kura nyingi zaidi atatangazwa
mshindi.
b)
Majina kumi na mbili ya wanachama yatapendekezwa na kupigwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu ili kupata wajumbe tano wa Halmashauri Kuu.
c)
Ikiwa kiongozi aliyechaguliwa
atajiuzulu au kuondolewa madarakani kwa sababu zozote zile Mkutano mkuu wa
dharura utaitishwa katika kipindi cha miezi mitatu (3) ili kufanya uchaguzi na
kujaza nafasi iliyowazi.
d)
Ikiwa kiongozi hatakuwepo katika
mkoa ambao chama kinaendeshea shughuli zake kwa kwa vikao vitatu mfululizo kwa
sababu za kikazi/masomo/ugonjwa au utalii mkutano mkuu wa dharura utaitishwa
ili kufanya uchaguzi mara baada ya kipindi hicho.
e)
Kura
zitapigwa wa siri chini ya usimamizi wa Mwenyekiti au Mwenyekiti wa muda atakaechaguliwa na
wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi.
SURA
YA SITA
MAJUKUMU
YA VIONGOZI WA CHAMA
13. VIONGOZI WAKUU NA MAJUKUMU YAO.
(1) KUTAKUA
NA MWENYEKITI WA CHAMA:
a)
Kuhakikisha kuwa Katiba inafuatwa.
b)
Kuongoza Mikutano.
c)
Kusimamia shughuli zote za utendaji wa Chama.
d)
Atawajibika kwa Mkutano mkuu ya Chama
e)
Atakuwa mtia saini katika akaunti ya fedha za chama.
f)
Atakuwa mtia saini katika mikataba yote inayohusu chama.
g) Atakuwa ndie
msimamizi mkuu wa shughuli zote za chama
(2) KUTAKUWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA.
a)
Ndiye atakae kuwa mtendaji mkuu wa shughuli za chama na atawajibika kwa Mwenyekiti wa Chama.
b)
Kuitisha na
kuandaa mikutano kwa mujibu wa katiba.Kutunza kumbukumbu na nyaraka zote za chama.
c)
Atapokea maombi ya Wanachama wapya na kuwasilisha kwenye Halmashauri kuu kwa kujadiliwa.
d)
Atapokea hoja mbalimbali za
wanachama na kuzifanyia kazi.
e) Kuwajulisha
kimaandishi wanachama waliofukuzwa na Mkutano Mkuu ama wale waliopoteza
uanachama kwa kutozingatia maagizo ya katiba kama ilivyoainishwa katika vifungu 9(1) (a) hadi 9(1) (g).
f)
Atakuwa mtia saini katika akaunti ya
fedha za chama.
(3)KUTAKUWA
NA MTUNZA HAZINA WA CHAMA.
a)
Kukusanya michango na kutunza
kumbukumbu za fedha.
b)
Kufanya malipo yaliyoidhinishwa kwa
mujibu wa katiba.
c)
Atawajibika kutayarisha bajeti ya
mwaka ya chama.
d)
Kutoa taarifa za mapato na Matimizi
ya fedha za chama katika mikutano yote.
e)
Atawajibika kutoa “bank statement” inayoonyesha mapato na
matumizi tokea mkutano mkuu wa mwisho ulipofanyika.
f)
Atakuwa mtia saini katika akaunti ya
fedha za chama.
g)
Atawajibika kwa Mwenyekiti wa chama kwa mujibu wa katiba.
14. VIONGOZI WAKUU WAANDAMIZI NA MAJUKUMU YAO.
(1) KUTAKUWA NA MAKAMU MWENYEKITI
a)
Kumsaidia Mwenyekiti na kufanya kazi
zote kama Mwenyekiti Hayupo.
b)
Endapo Mwenyekiti atajiuzulu au
kuondolewa madarakani kwa sababu zozote zile, Makamu Mwenyekiti atakaimu nafasi
hiyo kwa mujibu wa kijifungu 12(d) cha
Katiba hii.
c)
Endapo Mwenyekiti hata kuwepo katika
vikao vitatu kwa sababu za kikazi/masomo/ugonjwa au utalii, Makamu mwenyekiti
atakaimu nafasi hiyo na mara baada ya kipindi hicho uchaguzi utafanywa kwa
mujibu wa kifungu 12(e) cha katiba
hii.
(2) KUTAKUWA NA MAKAMU KATIBU MKUU.
a)
Kumsaidia Katibu Mkuu katika
majukumu yake yote.
b)
Endapo Katibu Mkuu atajiuzulu au
kuondolewa madarakani kwa sababu zozote zile, Makamu katibu mkuu atakaimu
nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu 12(d) cha
Katiba hii.
c)
Endapo Katibu Mkuu hatakuwepo katika
vikao vitatu mfululizo kwa sababu za kikazi/masomo/ugonjwa au utaliii, Katibu
Msaidizi atakaimu nafasi hiyo na mara baada ya kipindi hicho uchaguzi utafanywa
kwa mjibu wa kijifungu 12(e) cha
Katiba hii.
d) Atawajibika
kwa katibu mkuu kwa mujibu wa katiba=
15. KIPINDI CHA KUWEPO MADARAKANI.
Baada ya
kuchaguliwa, viongozi watakaa madarakani kwa vipindi (Viwili/mitatu/mine/mitano) iwapo kiongozi atashinda katika uchaguzi
wa awamu nyingine.
16. HALIMASHAURI KUU YA CHAMA
(1) WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU;
a)
Mwenyekiti
b)
Katibu mkuu
c)
Mweka
Hazina.
d)
Makamu
Mwenyekiti.
e)
Katibu
Msaidizi.
f)
Wajumbe tano (5) watakaochaguliwa na Mkutano
Mkuu wa Chama.
(2) KAZI ZA HALMASHAURI KUU
a)
Watasimamia na kutekeleza majukumu
yote kama yatakayoamuliwa na Mkutano Mkuu.
b)
Kubuni sera za chama na kutoa dira
ya chama ili kudumisha uhai Wake.
c)
Kuwajadili
wanachama wapya na kupeleka mapendekezo mbele ya Mkutano Mkuu.
d)
Kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote
na kumchukulia hatua za Kisheria itakapobidi kwa makubaliano ya wajumbe
wasiopungua theluthi mbili.
e)
Kuwasilisha mapendekezo ya kufukuzwa
kiongozi au viongozi waliosimamishwa mbele ya Mkutano Mkuu.
f)
Kuwasimamisha uanachama watu
watakaokiuka katiba na kupeleka mapendekezo ya kuwafukuza uanachama mbele ya
Mkutano Mkuu.
17. KAMATI ZA UTENDAJI NA KAZI ZAKE
(1) Kutakuwa na
Kamati mbili za Utendaji za Halmashauri Kuu ya Chama ambazo ni
a)
Kamati
ya fedha na uchumi, kamati hii itakuwa na wajumbe sita na itawajibika kwa Mwenyekiti wa Chama. Wajumbe watakuwa
Katibu Mkuu, Mweka hazina na wajumbe watatu wa halmashauri kuu.
b)
Kamati ya ustawi wa jamii na sherehe.kamati hii itaongozwa na wajumbe
halmashauri kuu,
(2) kazi kuu ya
kamati ya ustawi wa jamii na sherehe hii
ni:-
a)
Kuhamasisha wanachama kutoa michango
inayowahusu
b)
Kuhamasisha wanachama kuwasaidia
wanachama walio wagonjwa mahututi.
c)
Kuhamasisha wanachama kushiriki
katika Harusi na sherehe za mwanachama.
d)
Kuratibu sherehe za kuadhimisha
mwaka kama ilivyoainishwa katika kifungu
7(1) (c) Cha katiba hii.
18. MIKUTANO YA CHAMA NA KAZI ZAKE.
a) Kutakuwa na
Mkutano Mkuu utakaofanyika mara moja kwa mwaka
b) Kutakuwa na
mkutano wa Halmashauri Kuu kila baada ya miezi miwili.
c) Kutakuwa na
mkutano wa wanachama wote kila baada ya miezi mitatu.
d) Kutakuwa na
mkutano wa uchaguzi mkuu mara moja
kila baada ya mwaka mmoja.
e) Mkutano wa
dharura unaweza kuitishwa endapo viongozi ama asilimia hamsini (50%) ya wanachama wataona ipo haja ya
kufanya hivyo.
19. KAZI ZA
MKUTANO MKUU.
a) Kupokea
taarifa mbalimbali za kiutendaji.
b) Kutoa
maamuzi yahusuyo uhai na ubora wa chama.
c) Kubadili
kifungu cha Katiba endapo itaonekana ni lazima kufanya hivyo.
d) Kuthibitisha
kuachishwa au kufukuzwa Uanachama mtu yeyote.
e) Kufanya
uchaguzi viongozi wa chama.
f)
Kuthibitisha kuachishwa au kufukuzwa
kwa kiongozi.
g) Kuthibitisha
uanachama wa mwombaji mpya.
h) Kuchagua
Viongozi wa ngazi za juu pamoja na Halmashauri Kuu.
SURA
YA SABA
FEDHA ZA
CHAMA.
20. UHIFADHI
WA FEDHA ZA CHAMA
(1) Fedha yote
ya chama itatunzwa katika Bank ambayo itateuliwa na wanachama wa chama hiki na
kusimamiwa na Mtunza Hazina.
(2) Chama
kitakuwa na watia saini katika Bank ambao ni Mwenyekiti, Katibu Mkuu na mweka
hazina.
21. VYANZO VYA MAPATO
(1) Upatikanaji wa fedha
a) Kiingilio
cha uanachama.
b) Ada
za kila mwezi za uanachama.
c) Michango
ya dharura.
d) Mauzo
ya mali za chama kama vile katiba.
e) Faini
mbalimbali.
(2) Chama kitaanzisha na kubuni miradi
ya kiuchumi na kutoa huduma kwa wanachama kwa kuwa na chama cha kuweka na
kukopa kitakachotoa mikopo kwa riba nafuu kwa wanachama wake.
22. UKUSANYAJI WA FEDHA ZA CHAMA
Mwanachama
ataweka fedha za kiingilio na michango mingine katika Bank na kuwasilisha hati
ya malipo ya Bank kwa Mweka Hazina na kupewa Stakabadhi.
23. MATUMIZI
YA MFUKO WA CHAMA
(1) Kutoa rambirambi kwa wafiwa kama
ilivyoainishwa katika kifungu cha 9 (2)
(a)
(2) Kugharimia shughuli za Mkutano
Mkuu kwa kiwango kilichoamuliwa na Mkutano Mkuu
(3)Kugharamia shughuli za Halmashauri kuu kwa kiwango kilichoamuliwa na
Mkutano Mkuu
(4)Kugharimia uchukuaji
na upelekaji wa fedha kwa mfiwa kwa
kiwango kilichoamuliwa na Mkutano Mkuu
(5)Kugharamia shughuli za msingi za
uendeshaji wa chama kama vile upashanaji
habari kupitia magazeti na redio, ununuzi wa karatasi, kalamu, stemp,
bahasha na kutoa nakala za taarifa za
chama. Usimamizi utakuwa chini ya Halmashauri
Kuu.
(6) Kugharamia shughuli za sherehe
za chama kwa 25% ya bajeti ya sherehe na
itavyopitishwa na Mkutano Mkuu.
24. UPASHANAJI TAARIFA
Mwanachama
mwenye taarifa ya msiba, Harusi, au ugonjwa atawajibika kutoa taarifa kwa
mjumbe wa halmashauri kuu, viongozi au wanachama walio karibu naye kwa njia
yoyote kwa lengo la kuwashirikisha wanachama.
SURA
YA NANE.
MAMBO
YA JUMLA YA KATIBA.
25.
KUBADILI
KATIBA,
Kwa kuwa katiba sio maandiko matakatifu,
wanachama kupitia taratibu zake wanaruhusiwa kuifanyia marekebisho ya
kuiongezea au kupunguza baadhi ya vipengele vilivyopitwa na wakati
26. USULUHISHI:
Migogoro ya ndani ya chama itapatiwa
usuluhishi na halmashauri kuu ya chama, endapo litashindikana kutatuliwa na
halmashauri kuu basi busara ya waasisi itatumika kutatua mgogoro huo.
26. KUFUTWA KWA
CHAMA(RESOLUTION);
Chama
hiki kitafutwa kwa maamuzi ya sheria za nchi na chama chenyewe ikiwa:Kama
kitatenda makosa yanayokiuka sheria za nchi, kama vile kwenda kinyume na sera
za vyama na sera ya taifa ya mashirika yasiyo ya kiserikali
27.
MALI ZA
CHAMA ENDAPO CHAMA KITAFUTWA.
(1)
Kuteua Mfilisi atakayesimamia namna
mali hizo zitakavyotumika au kuzigawa,
(2)
Kulipia madeni ya chama kabla ya
kuanza kugawa au kuhamishiwa kwa asasi nyingine za walengwa
TAMKO RASMI
LA MKUTANO MKUU WA KWANZA ULIOFANYIKA TAREHE 31/08/2014 NA MAREKEBISHO YA
KWANZA YA KATIBA YALIYOFANYIKA TAREHE__________________.
Katiba hii ni halali na mali ya
chama
Katiba hii itatumika Kwa ushahidi wa
kisheria.
Badiliko lolote litakalofanywa na
mkutano mkuu litaheshimiwa na viongozi
na wanachama.
Chama.
MWISHO
KANUNI ZA UENDESHAJI WA CHAMA
UTANGULIZI
Mkutano mkuu wa UWAKISE
uliofanyika tarehe …… na ule wa tarehe_________ uliamua kwa kauli moja kuwa
baadhi ya vipengele katika katiba viwekewe na kuboresha Kanuni zilizopo.
Kanuni hizi zinaweza kufanyiwa marekebisho na mkutano
mkuu wa UWAKISE pale inapobidi na
zitaendelea kutumika mpaka tarehe ambayo mkutano mkuu wa UWAKISE utakapoamua vinginevyo.
Madhumuni ya Kanuni hizi ni kutoa mwongozo kwa
viongozi na wanachama katika kutekekeza wajibu wao kwa chama kwa jumla.Kanuni
zinalenga katika maeneo ambayo yanaweza yakapitwa na wakati katika kiipindi
kifupi kama vile ada ya kujiunga na uanachama, ada ya kila mwezi na kiasi cha
fedha zitakazotolewa kwa mwanachama kama rambirambi atakapopata msiba. Aidha,
Kanuni zinafafanua adhabu/faini atakayopewa mwanachama anapoenda kinyume na
katiba. Kuwepo kwa kanuni kutasaidia kuwa na katiba imara ambayo haifanyiwi
marekebisho ya mara kwa mara na hivyo kujenga mazoea ya kufanya hivyo.
Kanuni hizi msingi wake mkuu ni katiba ya UWAKISE na si vinginevyo.
WAJIBU WA MWANACHAMA
KWA CHAMA
Katika kuhakikisha kuwa chama kinakuwa hai na
kinatekeleza majukumu yake kikamilifu, na kwa kuzingatia kifungu kikubwa Na. 9 cha katiba ya UWAKISE, na kufafanuliwa na vifungu vidogo Na. 9(1) (a) na 9(1) (b) vya katiba hiyo pamoja na mambo
mengine, mwanachama atatakiwa kutekeleza mambo yafuatayo:
i)
Kulipa kiingilio ambacho ni Tsh. 50,000/=
ii)
Kulipa ada ya uanachama ya kiasi cha
Tsh. 5,000/= kila mwezi
Mwanachama
atakuwa na uhuru wa kulipa kwa miezi yoyote anayotaka au mwaka mzima au zaidi.
iii)
Kwa mujibu wa kifungu No. 9(1) (d) hadi 9(1) (g) vya katiba hiyo mwanachama
anawajibika kuhudhuria vikao vinavyo mhusu bila kukosa
asipohudhuria
kikao bila kutoa taarifa maalum kwa katibu au katibu msaidizi atawajibika
kulipa faini ya shilingi 3,000/=
(Elfu tatu tuu).
iv)
Atakayechelewa kufika kwenye kikao
nusu saa baada ya muda uliopangwa atatozwa Tsh. 2000/= (Elfu moja).
v)
Asipolipa faini zilizotajwa katika
vifungu (iii) na (iv) hapo juu, fedha hizo zitakatwa
kwenye malipo yake ya ada ya kila mwezi.
vi)
Ataachishwa uanachama ikiwa
hatahudhuria mikutano minne mfululizo
inayohusu bila sababu za msingi.
WAJIBU WA
CHAMA KWA WANACHAMA
Kufuatana na kifungu No. 4.0 cha Katiba ya UWAKISE
na kufafanuliwa na kijifungu kidogo Na..4.2.1
cha Katiba hii, ili kupunguza makali ya msiba, chama kitatoa rambiramni katika
misiba ifuatayo:
i)
Endapo mwanachama ataoa au kuolewa cha kitatoa Tsh. 500,000/=
ii)
Endapo mwanachama atafariki chama
kitatoa Tsh. 800,000/=
iii)
Kufiwa na Mume/Mke/Mtoto, chama
kitatoa rambirambi ya Tsh. 500,000/=
(Laki tano tu).
iv)
Kufiwa Baba/Mama, chama kitatoa rambirambi ya Tsh. 400,000/=
(Laki nne
tu)
v)
Kwa misiba ya Baba au Mama mzazi
inayohusu wanachama zaidi ya mmoja chama kitatoa huduma kwa kila mwanachama, kwani uanachama si wa
familia ya baba au mama mmoja ila ni wa mwanachama na familia yake( mume na
mke.)
MATUMIZI YA
MFUKO WA CHAMA
Kifungu Na. 9.4.2
hadi 9.4.6 cha Katiba ya UWAKISE,
mbali na misiba, kinaainisha maeneo mengine ambayo fedha za chama zitatumika.
Maeneo hayo na gharama zake ni kama yafuatayo:-
i)
Katika sherehe za chama za mwaka, mfuko wa chama utachangia kiasi
kilichopungua.
ii)
Kugharamia shughuli za mkutano mkuu, kwa kiwango kisichozidi Tsh. 120,000/=
iii)
Vikao vya chama/miktao ya dharura
kwa kiwango kisichozidi 50,000/=
iv)
Kugharamia
shughuli za Halmashauri kuu, kwa kiwango kisichozidi Tsh. 50,000/=.
v)
Kugharamia shughuli za Kamati ndogo za Halmashauri kuu, kwa kiwango
kisichozidi Tsh. 25,000/=.
vi)
Kugharamia uchukuaji na upelekaji pesa kwa Mfiwa kwa kiwango
Kisichozidi Tsh. 30,000/=
vi) Kugharamia ununuzi wa karatasi, kalamu, stamp,
bahasha, kutoa nakala za taarifa za chama na mawasiliano ya simu kama itatokea.
MWISHO
|
DAR ES SALAAM
FOMU YA MAOMBI
YA UANACHAMA
Mimi………………………………………wa Mtaa………………………………
P. O.
Box………………………….
Ninaomba
kujiunga na Chama cha UWAKISE, umri wangu ni
miaka
……..nimeoa / nimeolewa / sijaoa /sijaolewa. Nipo tayari kufuata taratibu za
chama kwa mujibu ya katiba ya chama hiki, na nipo tayari kutoa kiingilio na
michango ya kila mwezi kama ilivyoanishwa katika katiba na kanuni za chama.
Nina watoto
wafuatao.
JINA UMRI JINA UMRI
1…………………………… ……. 2…………………………. ……..
3…………………………… ……. 4…………………………. ……..
5…………………………… ……. 6………………………… ……..
Mimi na Mke/Mme
wangu kwa hapa DSM tunaishi…………………………..
Wazazi wetu
wapo hai / hawapo hai.
Baba na mama
Mzazi anaishi…………………………………….pia baba na mama mkwe
wanaishi…………………………………………………………….
UTHIBITISHO WA MUOMBAJI.
Ninathibitisha
kwamba yote niliyoeleza katika fomu hii ni ya kweli tupu.
Ninahidi kutoa
kiingilio cha Tshs…………………..na ada ya
kila mwezi kwa kipindi cha miezi………………ambayo ni Tshs………………..
Sahihi na
tarehe ya Muombaj………………………………………………….
Imepitishwa /
Haikupitishwa kwa sababu…………………………………………
……………………………………………………………………………………………..
NB: Endapo kama
nitafariki au kupatwa na tatizo mtu wangu wa karibu au mwakilishi wangu ni
………………………………. Ambaye ni …………………………………. Kwangu.
_____________________ _____________________
Sahihi ya Katibu Mkuu. Sahihi ya
Mwenyekiti
*Maombi yenye
taarifa ya uongo haitapitishwa,
(Gharama ya fomu hii ni Tshs 1000/= tuu- zijazwe nakala mbili) (Ambatanisha